Consta same Bagalwa, mkaazi wa Ituri ameiambia Sauti ya Amerika kwa njia ya simu kuwa katika shambuluo hilo raia wa China na mlinzi wake wa mgodi wa Muholo ulioko katika eneo la msitu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
“Hii si mara ya kwanza kwa raia wa China kuuawa na kushambuliwa mkoni Ituri ambako Wachina wapo katika misitu kuchimba madini ya dhahabu kwenye misitu na vijiji ambavyo havina barabara wala hospitali hata hakuna shule nzuri.”
Mkaazi mwingine wa Ituri Constan Same Bagalwa naye amesema “Utafahamu kwamba raia kutoka china wana jishughulisha na uchimbaji wa madini kimangendo katika sehemu nyingi za Congo bila kujadiliana na raia wa mahali ama kuwajengea hospitali lakini wakipata ulinzi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vya Congo, hasa hasa jeshi tiifu kwa serikali.”
Akizungumza kutoka Bunia, Diedone Losa, mratibu wa shirika la kiraia liloloko Ituri amesema shambulio hilo si la mara ya kwanza kutokea katika mkoa huo ambao una makundi mengi ya watu wenye silaha.
Vyombo vya usalama vimeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Imetayarishwa na Austere Malivika, Sauti ya Amerika, Goma