Wapatanishi wanatarajiwa kukutana leo Jumanne nchini Qatar kujaribu kukamilisha pendekezo la kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas.
Mazungumzo hayo yanakuja baada ya miezi 15 ya mapigano na kile watu wanaofahamu mazungumzo hayo walisema yalikuwa mafanikio kwa wiki hii katika juhudi za kumaliza vita huko Gaza.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Joe Biden alisema Jumatatu kwamba makubaliano yalikuwa yanakaribia kuzaa matunda. Katika hotuba yake kwa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ili kuangazia mafanikio yake ya sera za kigeni, Biden alisema makubaliano hayo yatawaachia huru mateka, kusitisha mapigano, kutoa usalama kwa Israel na kuturuhusu kuongeza msaada wa kibinadamu kwa Wa-palestina ambao waliteseka sana katika vita hivi ambavyo Hamas ilivianzisha.
Vigezo vya msingi vya pendekezo la kusitisha mapigano vitashuhudia mchakato huo ukijitokeza katika hatua kadhaa.