Mazungumzo ya kumaliza vita nchini Sudan yataendelea wiki hii

Wakaazi wa Sudan waliokoseshwa makaazi kufuatia mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF yamesababisha vifo na uharibifu wa mali kwa jamii.

Mazungumzo ya kumaliza miezi 15 ya vita nchini Sudan kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yataendelea mjini Geneva wiki hii, mjumbe maalum wa Marekani, Tom Perriello alisema leo Jumatatu.

Haijabainika wazi iwapo ujumbe wa jeshi la Sudan au serikali utajiunga na mazungumzo hayo.