Mazungumzo ya Syria nchini Uswisi

A rebel fighter from Jaysh al-Sunna, operating under a coalition of rebel groups called Jaish al-Fatah, or the army of conquest, prepares his weapon.

Makamanda wa uasi pamoja na wapinzani wa kisiasa huko Syria wamekiri kuwa juhudi zao za kijeshi dhidi ya Rais Bashar al Assad haziwezi kushinda licha ya usaidizi wa kijeshi kutoka nchi za Russia na Iraq.

Hata hivyo wamesema kuwa utawala huo wa Assad hauna uwezo wa kuangamiza au hata kumaliza uasi. Mizozo ilioko Syria imeligawanya taifa hilo katika makundi bila kuwa na dalili za kupata suluhisho la kisiasa la kulinganisha taifa.

Wanadiplomasia wa Marekani wameendelea kusihi wapatanishi kutoka makundi ya waasi kukubali kuunda serikali ya muungano ya mpito pamoja na Rais Assad lakini wamepuuzilia mbali wazo hilo.

Duru ya tatu ya mazungumzo ya amani mjini Geneva ilimalizika ghafla mwezi uliopita baada ya serikali kushindwa kukubaliana na upinzani kuhusu maswala muhimu.