Poland na mataifa 20 ya NATO yaanza mazoezi ya kijeshi

Poland na mataifa wanachama zaidi ya 20 wa NATO wameanza mazoezi ya kijeshi ya kiwango kikubwa mapema leo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzihakikishia nchi za Ulaya ya kati na mashariki kutokana na wasiwasi wa vitendo vya Urusi karibu na Ukraine.

Kwa upande wa ikulu ya Urusi, Kremlin imepinga rasmi mazoezi hayo mapema leo kwa kusema hawachangii chochote mustakabali wa uaminifu na usalama wa bara hilo.

Hali ya mvutano baina ya Urusi na mataifa ya magharibi imekuwa ya juu kuliko ilivyokuwa toka kumalizika kwa vita baridi.

Japokuwa Urusi inaipinga NATO kupanuka katika mataifa ya zamani ya Urusi, katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amehakikisha kwamba “vita baridi ni historia na wanataka ibaki kuwa hivyo.”