Marais wa nchi za maziwa makuu na SADC waunga mkono mkataba wa Kinshasa

Balozi Augustine Mahiga waziri wa mambo ya nje wa Tanzania.

Marais wa nchi za kanda ya maziwa ICGLR na wale wa jumuiya ya SADC wameunga mkono mkataba wa kisiasa uliotiwa saini mjini Kinshasa wiki iliyopita na ambao unaongeza muda wa rais Kabila kuendelea kubaki madarakani hadi April 2018.

Marais hao wamezungumzia pia hali ya kisiasa nchini Burundi, Jamhuri ya Afrika ya kati na Sudan Kusini.

Viongozi hao pia wamelaani machafuko yaliotokea jijini Kinshasa Septemba 19, 20 mwaka huu na kutaka kuwe na amani ya jkudhumu nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Agustine Mahiga katika mahjiano na VOA amesema nchi za maziwa makuu ambazo zina matatizo yanayofanana lakini Congo ni zaidi na walikuwa wakijadili nchi hiyo kwa undani zaidi.

Marais hao hawakueleza tofauti ya upinzani na kabila itakavyopewa ufumbuzi wakisema yale ya muhimu yanayotakiwa kwasababu ya muhimu yanaweza kuzungumzwa na kazi bado inaendelea.

Kila mtu anahusika katika hili SADC tupo karibu zaidi na DRC kwasababu ni wanachama lakini au tuko mbele zaidi baada ya kumtuewa Edem kojo kuwa msimamizo aliongeza waziri Mahiga.