Qatar siku ya Ijumaa imefanya shughuli za mazishi ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh baada ya mauaji yake mjini Tehran, shambulizi lililolaumiwa Israel ambalo limeongeza hofu ya kuongezeka mzozo wa kikanda.
Haniyeh, mkuu wa kisiasa wa kundi lenye silaha la Palestina, alikuwa akiishi Doha pamoja na wajumbe wengine wa ofisi ya kisiasa ya Hamas.
Amezikwa kwenye makaburi huko Lusail, kaskazini mwa mji mkuu wa Qatar, baada ya swala ya mazishi katika msikiti wa Imam Muhammad bin Abdul Wahhab, ambao ni mkubwa zaidi wa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.