Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi tajiri 7 duniani G7, wamekutana leo Jumamosi kwa mazungumzo kuhusu mgogoro wa mashariki ya kati.
Wanazungumzia pia vita nchini Ukraine wakati kipindi cha baridi kinakaribia.
Italy, ambayo inaongoza muungano wa G7, ni mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi, mjini Naples, makao makuu wa NATO.
Waziri wa ulinzi wa Italy Guido Crosetto, amewakaribisha washirika wakiwemo mkuu wa NATO Mark Rutte na mkuu wa sera ya mambo ya nje wa umoja wa Ulaya Josep Borrell.
Wanazungumzia uvamizi wa Russia nchini Ukraine, hali ya vita mashariki ya kati na ukosefu wa utulivu katika jangwa la sahara.