Mauaji ya polisi 5 katika mji wa Dallas, Texas hapa Marekani jana usiku ni moja wapo ya mauaji mabaya kwa polisi katika kipindi cha miaka 100 na kuweka historia nyingine mbaya ya mauwaji wa polisi tangu shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001.
Wakati huohuo mkuu wa polisi wa Dallas mapema leo washukiwa watatu wamekamatwa na idara husika zinasema mshukiwa wa nne amekufa saa kadhaa baada ya maandamano ya amani kupinga mauaji ya wanaume wawili weusi yaliyofanywa na polisi weua yalizozua kadhia.
Polisi walifanya mazungumzo ya muafaka na mshukiwa wa nne kabla ya kuanza kufyatuliana risasi katika doria iliyowekwa katika sehemu moja katikati ya mji huo.
Haijulikani kama mtu huyo alijifyatulia risasi mwenyewe ama aliuwawa na polisi.
Rais wa Marekani, Barack Obama, mapema leo amesema mashambulizi ya leo yalikuwa hayana maana, yaliyopangwa na mashambulizi ya chuki.