Wachunguzi wa Umoja wa mataifa wamepata taarifa zaidi kuhusu mauaji ya halaiki ya watu yaliyotekelezwa na kundi la wahalifu la Wharf Jérémie mjini Port-au-Prince, Haiti, mapema mwezi huu.
Ripoti ya Pamoja iliyochapishwa na ofisi ya umoja wa mataifa nchini Haiti na ofisi ya mkuu wa tume ya haki za kibinadamu, inasema zaidi ya watu 207 waliuawa kati ya Desemba 6 na 11.
Idadi kubwa ya waliouawa walikuwa watu wazee walioshutumiwa kwa uchawi na kusababisha magonjwa yaliyoepelekea mtoto wa kiongozi wa kundi hilo la wahalifu kuugua.
Wengine waliouawa ni wale waliokuwa wanajaribu kutoroka na wanaodaiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Ripoti hiyo inasema zaidi ya watu 5,350 wameuawa na zaidi ya 2,155 kujeruhiwa kutokana na ghasia za wahalifu nchini Haiti.