Mauaji na hasira Palestina kufuatia msako wa wanajeshi wa Israel

Wanafunzi wa Palestina wakikabiliana na maafisa wa usalama wa Israel Aug 6, 2022

Maafisa wa afya wa Palestina, wamesema kwamba wanajeshi wa Israel wamepiga risasi na kumuua kijana wa kipalestina wakati wa ukamataji mapema Jumatatu asubuhi uliopelekea mapambano katika kambi ya wakimbizi nje ya mji wa Jericho, katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi.

Wizara ya afya ya Palestina imesema kwamba Jibril Kamal, mwenye umri wa miaka 17 alifariki baada ya kupigwa risasi kichwani.

Darzeni ya wapelestina wamebeba mwili wa Kamal na kuandamana mjini Jericho wakiomboleza.

Watu wengine sita wamejeruhiwa wakati wa uvamizi huo, watu watatu kati yao wamejeruhiwa vibaya.

Jehsi la Israel limesema kwamba wanajeshi wake wamewapiga risasi washukiwa waliowashambulia wakati wa msako katika kambi ya wakimbizi ya Aqabat Jabr, na kwamba watu waliokuwa wamelengwa walitambuliwa.

Msako huo wa mjini Jericho umefanyika wakati ambapo msako umekuwa ukiendelea huko Ukingo wa Magharibi ukimalizika kwa washukiwa 17 kukamatwa na silaha kadhaa kupatikana.