“Tumekuwa na mawasiliano ya awali na RSF. Tumekuwa na mawasiliano ya kina na jeshi la Sudan( SAF). Lakini bado hawajatupa uthibitisho, ambao ungekuwa muhimu leo ili kusonga mbele Agosti 14,”, Tom Perriello, mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Sudan, aliwambia waandishi wa habari mjini Geneva Jumatatu.
Perrielo alisema “Tutasonga mbele na washirika wetu wa kimataifa kufikia mpango wa utekelezaji, mpango wa utekelezaji madhubuti kuhusu jinsi gani tunaweza kusonga mbele hadi kukomesha ghasia na kupata usambazaji kamili wa misaada ya kibinadamu, na utaratibu wa ufuatiliaji wa utekelezaji. Mambo haya yalikuwa yafanyike muda mrefu uliopita.”
Umoja wa Mataifa unauchukulia mzozo wa Sudan kama mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani. Mzozo huo mbaya ambao umeikumba Sudan umesababisha zaidi ya watu milioni 10.7 kuwa wakimbizi wa ndani ya nchi na kuwalazimisha wengine milioni 2 kukimbilia nchini jirani kutafuta hifadhi.