“Wafanyakazi, wasomi na watu wenye ujuzi walichukuliwa kutoka hapa. Hivi leo, tunahitaji nguvu kazi hii ambayo ilikuwa na ujuzi ili Afrika iweze kusonga mbele na kufikia hali bora zaidi.” - Isilda Hurst, Mwanahistoria.
Mwaka 2019 ni maadhimisho ya miaka 400 tangu Waafrika wa kwanza kufanywa watumwa kuwasili nchi ambayo leo ni Marekani.
Kuwasili kwa meli iliyokuwa imewabeba Waafrika kutoka Angola katika koloni la Virginia, mwezi Agosti 1619, ilikuwa ni mwanzo wa kuanza biashara ya utumwa iliyodumu kwa zaidi ya miaka 200 nchini Marekani.
Mayra de Lassalette na Betty Ayoub wa VOA walisafiri hadi Angola kufahamu zaidi kuhusu chanzo kimojawapo cha biashara ya watumwa waliovushwa bahari ya Atlantic na athari zinazoendelea katika eneo hilo.