Matokeo ya awali uchaguzi Uganda yaonyesha Museveni anaongoza

Rais Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anaongoza katika uchaguzi wa rais uliofanyika Alhamisi.

Anaongoza kulingana na matokeo ya awali ambayo yametangazwa Ijumaa na tume ya uchaguzi, huku mpinzani wake mkuu Bobi Wine akisema ana ushahidi kwamba uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura.

Kwa karibu asilimia 30 ya kura zilizo hesabiwa Alhamisi, Museveni alipata kura millioni 1,852,000 sawa na asilimia 63.9, naye Bob Wine alipata kura laki 821,000 sawa na asilimia 28.4, tume ya uchaguzi nchini Uganda imesema.

Bobi Wine, mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa na kuwahamasisha vijana kwa ajili ya mababiliko ya kisiasa, leo ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba alipiga picha ya udanganyifu uliofanyika wakati wa kupiga kura, na kuongeza kuwa anataka matokeo ya amani ya kura.

Mapema leo, Wine ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba ana imani ameshinda uchaguzi licha ya wizi mkubwa wa kura na vurugu.