Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:15

Uganda yakataa kutoa vibali kwa waangalizi wa Marekani kufuatilia uchaguzi


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Marekani imetangaza kwamba haitatuma waangalizi kufuatilia uchaguzi mkuu wa Uganda utakaofanyika Kesho alhamisi.

Hii ni baada ya asilimia 75 ya maafisa wake kunyimwa vibali vya kufuatilia uchaguzi huo.

Balozi Natalie Brown amesema kwamba tume ya uchaguzi ya Uganda haijatoa sababu yoyote ya kukataa maombi hayo licha ya juhudi kadhaa za kutaka maelezo kutoka kwa ubalozi wa Marekani nchini Uganda.

Brown amesema kwamba waangalizi wa kutoka ubalozi huo, ambao wengi wao ni raia wa Uganda, wamenyimwa fursa ya kutumikia raia wenzao.

Amesema hatua hiyo itapelekea uchaguzi wa Uganda kukosa uwazi, Imani na uwajibikaji.

Wakati huo huo, Marekani imeshutumu hatua ya serikali ya Uganda kuzima mitandao yote ya kijamii, wakati nchi hiyo inaandaa uchaguzi mkuu, huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres akitoa wito kwa utawala wa Uganda kuheshimu haki za kibinadamu.

Guterres ametaka serikali na wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kujizuia na uvunjani wa sheria na vitendo vinavyoweza kuchochea ghasia.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ameshutumu kampuni zinazomiliki mitandao ya kijamii hasa Facebook na twiter, kwa kile ametaja kama majivuno na upendeleo, akisema kwamba ameamurisha zifungwe nchini humo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG