Mshindi wa uchaguzi wa rais Kenya kutangazwa Ijumaa

Wawakilishi wa vyama mbali mbali na maafisa wa uchaguzi wakijadili wakati wa kuhibitisha matokeo ya uchaguzi wa rais kwenye makao ya kuhesabu kura, Bomas Nairobi.

Matangazo rasmi ya mwisho ya matokeo ya uchaguzi wa rais Kenya yanatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa baada ya kujumwisha matokeo ya wilaya zote za uchaguzi kufuatana na Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Isack Hassan.

Taarifa hiyo ilitolewa Alhamisi jioni baada ya utaratibu wa kutangaza kura kusitishwa kwa saa mbili na kjzusha wasi wasi mpya miongoni mwa wananchi kwamba huwenda Tume Huru ya Uchaguzi IEBC italazimika kusitisha kazi za kujumisha matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka maeneo bunge yote, ikiwa CORD itafanikiwa na malalamiko yake mahakamani.

Akizungumza na waandishi habari Alhamisi jioni Bw. Isack Hassan alisema kinyume na uvumi uloenea kwamba mfumo wa komputa na mawasiliano yameingiliwa na watu wa nje yani “Hackers” mfumo wa mawasiliano ya kutoa matokeo uko chini ya ulinzi thabiti.

Your browser doesn’t support HTML5

Matokeo kutangazwa Ijumaa


Akizungumzia malalamiko mengine ya CORD kwamba kuna maeneo ambayo wapigaji kura walikuwa wengi kuliko waloandikishwa. Bw Hassan alisema.

“Hadi hivi sasa tume haijashuhudia mahala ambapo wapigaji kura ni wengi kuliko waloandikishwa na jambo hilo likitokea kura za wilaya hiyo ya uchauzi zinatupiliwa mbali. Baada ya taarifa hiyo matokeo yaliendelea kutolewa."

Wakati tulipokuwa tunaandika makala haya, Uhuru Kenyata wa munagno wa Jubilee alikuwa na kura milioni 3, 701, 055 nae Raila Odinga alikuwa na kura milioni 3, 401 499.

Wachambuzi wa kisiasa hapa Nairobi wanatoa msimamo takriba sawa kuwa inabidi wanasiasa waiwachie tume ya uchaguzi kuendelea na kazi zake na ikiwa wanamalalamiko basi wafikishe mahakamani.

Profesa Kimani Njogu wa kundi la shrtika lisilo la kiserikali Tuvuke anasema, “Ni lazima kwa wanasiasa waiwachie tume ya uchaguzi ikamilishe kazi yake na kulingana na katiba wana siku saba kuwasilisha malalamiko yao mbele ya mahakama kuu ili kusikilizwa.”

Wakati Wakenya wakisubiri matokeo ya rais kutangazwa ambayo huwenda yakatolewa Ijuma asubuhi kufuatana na mwenyekiti Hassan wakazi wa maeneo mbali mbali wamekuwa wakisherekea siku nzima ushindi wa magavana, wabunge na maseneta wao.