Maafisa kadhaa wa Ulaya wameelezea wasi wasi wao kwamba hatua ya kuchukuliwa kwa serikali hiyo na Taliban huenda ikaongeza ugaidi pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi barani humo.
Uingereza na washirika wengine wa NATO walianza kuondoa raia wao kutoka nchini humo Jumapili, wakiandamana na mamia ya raia wa Afghanistan waliofanya kazi pamoja.
Mataifa mengine ambayo yanaendelea kuondoa raia wao ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani, Uhispania na Italia, baada ya Marekani kuchukua tena udhibiti wa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Kabul ulioshuhudia ghasia mwishoni mwa wiki.
Mataifa mengi ya Ulaya yanatarajiwa kutangaza programu zao za dharura ili kutoa hifadhi kwa raia wa Afghanistan walioko kwenye hatari kutokana na kushirikiana nao katika miongo miwili iliyopita.