Mataifa yenye nguvu duniani yatatathmini hali ya baadae ya Iran kuhusu nyuklia

Mazungumzo ya kufufua mapatano ya nyuklia ya Iran yalianza Alhamis

Mazungumzo ya kufufua mapatano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 yalianza tena siku ya Alhamis huku Marekani na Israel zikizidisha shinikizo la maneno dhidi ya Tehran kuhusu madhara yanayoweza kutokea kiuchumi au kijeshi iwapo diplomasia itafeli

Mataifa yenye nguvu duniani yatatathmini katika siku chache zijazo ikiwa Iran ina nia ya dhati wakati wa mazungumzo ya nyuklia baada ya kuashiria kuwa iko tayari kuendelea na mazungumzo kufuatana na hati zilizokubaliwa katika duru ya mwisho ya mwezi Juni, afisa mmoja wa ulaya ulaya amesema leo Ijumaa.

Mazungumzo ya kufufua mapatano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 yalianza tena siku ya Alhamis huku Marekani na Israel zikizidisha shinikizo la maneno dhidi ya Tehran kuhusu madhara yanayoweza kutokea kiuchumi au kijeshi iwapo diplomasia itafeli.

Mfano wa jengo la kiwanda cha nyuklia cha Tehran.

Mpatanishi mkuu wa Iran alisema Tehran inashikilia msimamo iliouweka wiki iliyopita, wakati mazungumzo hayo yalipovunjika na maafisa wa ulaya na Marekani, wakiishutumu Iran kwa kutoa matakwa mapya na kukataa maafikiano yaliyotekelezwa mapema mwaka huu.

Iran ilisema ilikubali kufanya kazi kutoka kwenye maandishi ya Juni. Hatua hii sasa itajaribiwa kwa siku kadhaa zijazo, chanzo kimoja kilisema, kikizungumzakwa sharti la kutotajwa jina.