Ahadi hiyo ni mojawapo ya zile zilizofanywa Alhamisi kwenye kikao cha Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa cha COP26 mjini Galsgow. Hata hivyo wakosoaji wanasema kwamba ahadi hizo siyo za kutegemewa kutokana na kwamba mataifa yanayotumia makaa ya mawe yakiwemo Marekani, China, India na Japan, hayajatoa ratiba ya kusitisha utumizi wake.
Baadhi ya wakosoaji wanasemekana kuandamana nje ya ukumbi wa mkutano wakipinga baadhi ya hatua zilizochukuliwa. Wanasema kwamba ahadi zilizotolewa zinatofautiana kwa kuwa baadhi ya mataifa yaliahidi kusitisha kabisa uzalishaji wa makaa ya mawe huku mengine yakiahidi kutojenga viwanda zaidi, wakati mengine kama China yakisema kwamba yatasitisha ufadhili wa viwanda vinavyotumia makaa hayo kwenye mataifa ya kigeni.
Uingereza imesema kwamba baadhi ya mataifa yaliyoahidi kusitisha utumiaji wa makaa hayo ni zaidi ya 20, yakiwemo Ukraine, Vietnam, Korea Kusini, Indonesia na Chile.