Mashirika ya kutetea amani Kenya yawataka wanasiasa kuwa na subra

Mgombea kiti cha rais Kenya Raila Odinga (kulia) na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka

Mungano wa mashirika 18 ya kutetea amani Kenya chini ya jina la Tuvuke umetoa taarifa ya kuwataka wanasiasa kutoingilia kati kazi za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC hadi imemaliza kazi zake za kuhesabu kura.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Profesa Kimani Njogu, anasema kufuatana na katiba ya Kenya wanasiasa wanasiku saba baada ya matokeo kutangaza kuwasilisha malalamiko yao mbele ya Mahakama Kuu ya nchi.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Profesa Kimani Njogu


Taarifa hiyo imetolewa wakati mgombea mwenza wa mungano wa CORD Kalonzo Musyoko kutangaza kamba mungano wao unaushaidi wa kuwepo na kasoro katika utaratibu wa uchaguzi na kamba kuna maeneo ya kati ambako wapigaji kura walikuwa wengi kuliko waloandikishwa.

Mwenyekiti wa IEBC Isack Hassan alisuta mara moja madai hayo na kusema jambo hilo likiwa limetokea basi kura za wilaya hiyo zinafutiliwa mbali.