Mashehe 4 wahukumiwa kifungo cha maisha, wawili miaka 30 Uganda

Mskiti wa mji wa Mubende Uganda

Mahakama ya uhalifu wa kimataifa jijini Kampala nchini Uganda, Jumanne imetoa kifungo cha maisha kwa mashehe 4 ambao wamekutikana na hatia ya ugaidi. Wawili wamepewa miaka kifungo cha miaka 30.

Mahakama hiyo pia imewaachia huru wengine 8 ambao hawakupatikana na makosa.

Mashehe hawa sita walikutwa hawana hatia ya mauaji.

Kamoga, pamoja na mashehe wenzake 13, walikuwa wanakabiliwa na makosa ya ugaidi, mauaji na jaribio la kuua, makosa mahakama iliwafungulia miaka mitatu iliyopita.