China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

China inaweka masharti ya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini kulingana na vikwazo vipya vikali vya Umoja wa Mataifa dhidi ya mpango wa nyuklia na makombora wa Pyongyang.

Beijing ilitangaza mapema leo kwamba itasitisha kupeleka mafuta ya ndege kwenda nchini humo, na itasimamisha ununuzi wa makaa ya mawe, dhahabu, titanium na madini mengine adimu kutoka kwa mshirika wake maskini.

China inasema itachukua baadhi ya hatua kwa vikwazo hivyo endapo tu bidhaa hizo zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kiraia na hazihusiani na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ama mpango wake wa makombora.