Mauaji ya raia yamefanyika wakati waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, akiitembelea Kyiv, kuonyesha uungwaji mkono.
Watu watatu walikufa na wengine 10 kujeruhiwa Ijumaa katika mapambano makali yaliyokuwa yakiendelea mkoa wa mashariki wa Donetsk, Gavana Pavlo Kyrylenko, alisema Jumamosi.
Maafisa wa Ukraine, wanasema mapigano makali yalikuwa yanaendelea katika maeneo matatu ya Donetsk ambako ilielezewa kuwepo na idadi kubwa ya wanajeshi wa Russia, wanaojaribu kulikamta eneo hilo.
Serekali kwenye mitandao ya kijamii ilisema maeneo ya Bakhmut, Lyman na Marinka, yanashuhudia mapigano na kwamba Russia, ilijaribu bila mafanikio Ijumaa kusonga mbele.
Watu watano, akiwemo mtoto walijeruhiwa Ijumaa na usiku kucha mapigano yaliendelea katika mkoa wa Kherson upande wa kusini, kulingana na Gavana Oleksandr Prokudin.