Mashambulizi ya Taliban kwa IS yaleta manufa

Kufanikiwa kwa Taliban katika mashambulizi dhidi ya tawi la Islamic State, Afghanistan, IS Khorasan, kwa kiwango kikubwa limeondoa heshima na kupunguza mashambulizi kwa raia kwa mujibu wa mwakilishi mwandamizi wa Marekani.

Tom West ambaye ni mwakilishi wa Marekani nchini Afghanistan ameelezea tathmini yake wakati wa warsha ya kituo kisicho fungamana na itikadi za kisiasa na kukutanisha wanazuoni jijini Washington.

Amesema hatua za kukabiliana na ugaidi zimepunguza kwa kiwango kikubwa mashambulizi kwa raia wa Afghanistan. Kumekuwa na mashambulizi mabaya dhidi ya watu wa kabila la Hazara, lakini toka kufanyika kwa juhudi hizo mashambulizi dhidi yao yamepungua aliongeza kusema.

Pamoja na kueleza hayo ameonya juu ya kundi la Tehrik-i-Taliban Pakistan kuweka tishio kubwa katika uthabiti wa kikanda.