Jeshi la anga la Israel limeripotiwa kushambulia ngome 40, ikiwemo miundombinu ya kijeshi na majengo yenye vilipuzi.
Hamas imeishtumu Israel kwa kuongeza mashambulizi yake ya hivi karibuni katika juhudi za kudhoofisha mpango wa sitisho la mapigano ambao Marekani imekuwa ikizishinikiza pande zote kuukubali. Israel inasisitiza kwamba mashambulizi hayo ni katika juhudi za kuitokomeza Hamas.
Katika tukio tofauti, maafisa wa Israel Jumanne walitangaza kwamba wataanza kutuma taarifa kwa wanaume wa Kiyahudi wafuasi wa vyama vya mrengo mkali vya Orthodox kupigana katika vita huko Gaza. Walikuwa hawaruhusiwi kupigana hadi pale Mahakama ya Juu ilipochukua uamuzi mwezi Juni.
Serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu inategemea vyama viwili vyenye siasa kali vya Orthodox katika muungano wake.
Uamuzi huo unatarajiwa kusababisha mvutano ndani ya nchi, na maandamano yalifanyika hapo awali wakati serikali ilipojaribu kusajili wanaume wa Kiyahudi wa Orthodox.