Shahidi huyo, Cheung Kim-hung, amesema Lai, anaamini kuwa sheria iliyopendekezwa ambayo itawaruhusu watu wa Hong Kong, kupelekwa China Bara kujibu mashtaka katika mahakama zinazodhibitiwa na chama cha kikomunisti itatumika kukandamiza demokrasia na uhuru wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa Cheung, Lai alisema jumuiya ya wafanyabiashara ilikuwa na wasiwasi endapo sheria ingepitishwa basi vyombo vya habari visingeweza kuendelea.
Mswaada huo baadaye uliondolewa na serikali.
Lakini maandamano makubwa juu ya mswaada huo yalibadilika na kuwa maandamano ya kuunga mkono demokrasia ambayo yalitikisa eneo hilo kwa miezi kadhaa.