Tamko la Hibatullah Akhundzada, linafuatia ripoti za karibuni za vyombo vya habari na picha za satelaiti zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Marekani, na kuthibitisha kwamba kilimo cha kila mwaka cha mazao ya afyuni kimepungua kwa kiasi kikubwa kwa taifa ambalo ni mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa mazao hayo.
Upunguzaji huo unatokana na agizo lililotolewa na mkuu wa Taliban, la Aprili 2022, ambalo lilipiga marufuku kabisa kilimo, uzalishaji, matumizi, usafirishaji, na uagizaji wa dawa zote haramu Afghanistan.
Marufuku hiyo iliruhusu vitengo vya kupambana na dawa za kulevya vya Taliban kutokomeza kilimo cha mauwa ya afyuni katika nchi hiyo maskini iliyoharibiwa na vita, ambayo ilichangia asilimia 85 ya uzalishaji duniani mpaka mwaka jana, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.