Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Martin Fayulu Jumamosi alithibitisha kugombea urais kwenye uchaguzi wa tarehe 20 Disemba.
Atashindana na rais Felix Tshisekedi, aliye madarakani tangu mwaka wa 2019, ambaye anawania muhula wa pili.
“Muungano wa Lamuka umeamua kuwasilisha ugombea wangu kwenye uchaguzi wa rais,” Martin Fayulu amewambia waandishi wa habari mjini Kinshasa.
Tangu Julai 2022, chama chake cha Ecide ambacho kinashiriki kwenye muungano wa Lamuka, kilikuwa kimemteua Martin Fayulu kuwa mgombea wake rasmi kwenye uchaguzi ujao wa rais.