Marekani iliibuka mshindi Jumapili katika michuano ya kombe la dunia la wanawake kwa kuwabwaga Waholanzi mabao mawili kwa sufuri kwenye fainali zilizofanyika kenye uwanja wa Stade de Lyon in Lyon, nchini Ufaransa.
Timu ya Marekani, ambayo ilikuwa inatetea taji lake, ilipata bao la kwanza kupitia penalti iliyopigwa na Megan Rapinoe mnamo dakika 61. Bao la pili lilifungwa na mchezaji Rose Lavelle dakika nane baadaye.
Rapinoe amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri wa juu zaidi (34) kufunga bao kwenye fainali za kombe la Dunia.
Hii ni mara ya nne kwa Marekani kushinda kombe la Dunia la soka ya Wanawake.
Kipa wa Uholanzi, Sari Van Veenendaal, anasifiwa na wachambuzi wa michezo kwa ustadi wake na jinsi alivyookoa mikwaju mikali iliyopigwa kwelekezwa kwenye wavu aliokuwa akilinda.
Michuano hiyo iiliendelea kwa mwezi mmoja tangu tarehe 7 mwezi Juni na ilishirikisha timu 24 kwenye fainali.