Marekani yazuia msaada wa kijeshi wa dola milioni 235 kwa Misri kutokana na ukiuakaji wa haki za binadamu

Mwenyekiti mpya wa kamati ya mahusiano ya nje kwenye Baraza la Seneti la Marekani, Ben Cardin

Mwenyekiti mpya wa kamati ya mahusiano ya nje kwenye Baraza la Seneti la Marekani jana Jumanne alizuia msaada wa kijeshi wa dola milioni 235 kwa Misri kutokana na wasi wasi wa haki za binadamu.

Ben Cardin alimwambia waziri wa mambo ya nje Antony Blinken kwamba ataendelea kuzuia ufadhili kwa Misri hadi nchi hiyo itakapopiga hatua ya kuridhisha kwenye sekta ya haki za binadamu.

“Ninaamini ni muhimu tuendelee kuiwajibisha serikali ya Misri na serikali zote kwa ukiukaji wao wa haki za binadamu,” Cardin alisema katika taarifa.

Alisema atazuia msaada huo kwa Misri wakati wote itakuwa “haijachukua hatua madhubuti na endelevu ili kuboresha hali ya haki za binadamu nchini humo.”

Cardin kutoka chama cha Rais Joe Biden cha Democratic, ameomba msamaha utolewe kwa baadhi ya wafungwa wa kisiasa wanaokadiriwa 60,000 nchini Misri.