Marekani, Jumatano imezuia azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likitaka kusitishwa kwa mapigano ya Gaza na kuachiliwa kwa mateka wa Israel, ikisema kuwa lugha iliyopendekezwa ingetuma ujumbe usio sahihi kwa Hamas.
“Marekani ilifanya kazi kwa wiki kwa nia njema ili kuepuka matokeo haya,” Naibu Balozi wa Umoja wa Mataifa, Robert Wood, amesema baada ya kupiga kura.
Ameongeza kusema kwamba waliweka wazi katika muda wote wa mazungumzo, juu ya kutounga mkono usitishaji mapigano vita bila masharti, ambao umeshindwa kuwaachilia mateka.
Kura ya turufu ya Marekani ilikuwa ya nne kwa Gaza toka vita kati ya Israel na Hamas kuanza miezi 14. Azimio lililoshindwa “linataka usitishaji vita wa mara moja, usio na masharti na wa kudumu likiheshimiwa na pande zote, na inasisitiza zaidi uhitaji wake wa kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote.