Hadi kufikia Jumamosi mashambulizi 201 ya bunduki kwa watu wengi yametokea kote Marekani mwaka huu, kwa mujibu Gun Violence Archive , tovuti inayofuatilia matukio ya ufyatuaji risasi nchini ambayo pia inafafanua kuhusu mashambulizi ya risasi ya pamoja ni tukio ambalo linahusisha watu wanne au zaidi wanapigwa risasi ukiachilia mshambuliaji mwenyewe.
Tovuti hiyo pia imeelezea kwamba zaidi ya watu 14, 700 wamekufa kutoka na ghasia za bunduki mwaka 2023 ambapo mashambulizi ya risasi ya watu wengi yamesababisha vifo vya watu tisa kwenye eneo la maduka katika jimbo la Texas Jumamosi ikiwa ni shambulizi kubwa la karibuni kulitikisa taifa.
Wakati huo huo kanisa la Cottonwood Creek lilishambuliwa kwa risasi Mei 7 huko Allen, Texas, wakati waumini walipokuwa wamekusanyika katika ibada ya faraja baada ya mtu aliyekuwa na silaha kuwapiga risasi watu wanane na kujeruhi takriban wengine saba katika Mall yenye harakati nyingi kaskazini mwa Dallas jumamosi.
Gavana wa texas Greg Abbott aliyeliita shambulizi hilo kuwa ni janga lisiloelezeka alihudhuria ibada hiyo.