Marekani yaunga mkono makubaliano ya kimataifa ya kupunguza uchafu wa plastiki baharini

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinke n. April 27, 2021. REUTERS/Leah Millis/Pool.

Marekani imeunga mkono mazungumzo kuhusu makubaliano ya kimataifa ya kupunguza uchafuzi wa plastiki, ambao unatishia uhai wa bahari na viumbe vya baharini duniani.

Marekani imeunga mkono mazungumzo kuhusu makubaliano ya kimataifa ya kupunguza uchafuzi wa plastiki, ambao unatishia uhai wa bahari na viumbe vya baharini duniani.

Wakati wa ziara yake katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP) mjini Nairobi, Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Marekani itaunga mkono makubaliano haya ambayo lazima yazingatiwe mwezi Februari mjini Nairobi.

Blinken alisema "Lengo lao ni kuunda zana ambayo itaweza kutumika kwa ajili ya kulinda bahari na viumbe vyote ndani yake kutokana na kuongezeka na tishio la kimataifa la uchafuzi wa plastiki”.

Mkataba huu pia utazingatia plastiki ndogo ndogo (chanzo cha uchafuzi wa mazingira ambao ukubwa wake ndio kwanza unaanza kupimwa) na ungekuza uchumi wa mzunguko unaojumuisha mzunguko mzima wa bidhaa hizi kutoka utengenezaji hadi matumizi yao. Linken anaelekea Nigeria hii leo kituo cha pili cha ziara yake ya nchi za afrika.