.Msaada huo mpya unajumuisha jumla ya msaada wa Marekani kufikia milioni 185 na utatolewa kwa mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali ambayo yameshiriki katika juhudi za uokoaji na ujenzi.
Waziri wa Marekani wa mambo ya nje Antony Blinken anaitembelea Uturuki kujionea mwenyewe uharibifu baada ya tetemeko lenye kipimo cha 7.8. Amesema msaada huo mpya utasaidia katika ununuzi wa blanketi, vyakula, nguo za joto, mahema na vifaa vya ujenzi wa makazi.
Msaada huo pia utaunga mkono huduma za afya na matibabu, juhudi za maji safi na usafi, na programu zinazounga mkono elimu ya watoto na vijana zilizoathiriwa na tetemeko hilo.
Blinken Jumapili alisafiri kwa helikopta katika baadhi ya maeneo yaliyoteketezwa na tetemeko hilo la ardhi na mwenzake wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu.
Blinken anatarajiwa kukutana na Rais Recep Tayyip Erdogan leo Jumatatu.