Mswaada huo wa ulinzi kwa mwaka 2023 ambao unahitaji kuidhinishwa na Baraza la Seneti na kusainiwa na Rais Joe Biden ili kuwa sheria, utaruhusu utoaji wa msaada kwa Taiwan hadi dola bilioni 2 kwa mwaka kuanzia mwaka 2023 hadi 2027.
Mswaada huo unamruhusu Biden kutoa hadi dola bilioni 1 kwa mwaka kama msaada wa vifaa vya kijeshi kutoka Marekani au huduma nyinginezo kama vile mafunzo ya kijeshi.
Beijing “imekuwa ikipinga vikali Marekani kutumia sheria ya taifa ya ulinzi kwa kupitisha maudhui mabaya kuhusiana na China,“ msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ching aliwaambia waandishi wa habari baada ya mswaada huo kupitishwa.
Beijing inadai Taiwan ni sehemu ya ardhi yake, ambayo itaunganishwa siku moja kwa nguvu, ikiwa itahitajika.