Marekani imetangaza Jumanne mipango kadhaa ya serikali na sekta binafsi iliyokusudiwa kuimarisha maendeleo na usalama katika Amerika ya Kati kama sehemu ya mpango ulioundwa kushughulikia sababu kuu za kwanini watu wanahamia Marekani.
Makamu wa Rais Kamala Harris amekuwa akiongoza mpango huo, ambao ulijumuisha kukutana na viongozi wa biashara Jumatatu usiku kabla ya kutangaza dola bilioni 1.9 katika miradi mipya ya kibinafsi kutoka kwenye biashara na mashirika 10.
Matangazo hayo yanakuja huku Marekani ikiwa mwenyeji wa viongozi wa Mkutano wa Wakuu wa Amerika wiki hii huko Los Angeles, lakini isipokuwa machache makuu.