Wizara ya fedha ya Marekani imesema katika taarifa kwamba hatua hizo zimelenga mali zaidi katika uwekezaji wa Hamas na watu wanaosaidia ukwepaji wa vikwazo kwa kampuni washirika wa Hamas.
Wizara hiyo imesema kampuni yenye makao yake Gaza ambayo ilisaidia kutuma fedha haramu za Iran kwa Hamas na kundi la Palestinian Islamic Jihad (PIJ) imelengwa pia na vikwazo hivyo.
Iran inaunga mkono Hamas na makundi mengine ya wanamgambo Mashariki ya Kati.
“Hatua ya leo inasisitiza dhamira ya Marekani ya kusambaratisha mitandao ya ufadhili ya Hamas kwa kuweka vikwazo vya kukabiliana na ugaidi na kufanya kazi na washirika wetu wa kimataifa ili kuwanyima Hams uwezo wa kutumia mfumo wa fedha wa kimataifa, naibu waziri wa fedha Wally Adeyemo amesema katika taarifa.