Ryder hakutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya wanajeshi waliopelekwa huko au kuhusu kile watakachofanya.
Hata hivyo, afisa mkuu wa Marekani ameiambia VOA kwamba ni darzeni ya wanajeshi na kazi yao ya kwanza itakuwa kujianda katika kusaidia raia wa Marekani kuondoka, iwapo vita vitazuka katika kanda hiyo yote.
Afisa mwingine wa Marekani amesisitiza kwamba hali haijafikia kiwango ambapo usaidizi wa jeshi kuwaondoa raia wa Marekani unahitajika.
Ikibidi kuwaondoa watu, jeshi la Marekani lina wanajeshi waliopelekwa eneo la karibu na watatekeleza kazi hiyo, afisa mwingine ameiambia VOA. Wote waliomba majina yao yasitajwe.