Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inawasihi Wamarekani kutosafiri kwenda Uingereza kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vipya vya COVID-19 nchini humo.
Wizara hiyo iliweka tahadhari ya usafiri kwenda Uingereza kwa kiwango cha juu Jumatatu, kufuatia hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Vituo vya Udhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Amerika mapema siku hiyo.
Taasisi zote mbili zilisema ikiwa ni lazima watu wasafiri kwenda Uingereza wahakikishe kuwa wamepewa chanjo zote kamili kabla ya safari yao
Ushauri huo uliofanyiwa marekebisho ulitolewa wakati watu wa Uingereza walisherehekea kile kilichoitwa "Siku ya Uhuru," ikiwa ni kuadhimisha mwisho rasmi wa karibu vizuizi vyote vya kufunga shughuli za kiuchumi pamoja na uvaaji wa lazima wa barakoa na umbali wa kijamii.