Marekani na nchi nyingine zaongeza ulinzi baada ya mashambulizi ya Boston
Polisi wa New York wakikagua begi la msafiri kwenye kituo cha Times Square kufuatia milipuko ya Boston, April 15, 2013.
Maafisa maalum wa SWAT wakifanya doria katika uwanja wa Copley baada ya milipuko karibu na sehemu ya kumalizia mbio za Boston Marathon April 15, 2013.
Bango limeweka kando ya barabara kutahadharisha operesheni za polisi wa Uingereza katika njia za mbio ndefu za London wiki ijayo.
Watalii wakipiga picha karibu na gari ya polisi wa Ujerumani wakilinda nje ya ubalozi wa Marekani mjini Berlin.
Maafisa wa FBI wakiwasili katika eneo la tukio karibu na sehemu ya kumalizia mbio ndefu za Boston, Massachusetts April 15, 2013.
Walinzi wa Malkia wakiwa mbele ya jumba la kifalme la Buckingham Palace wakiwa juu ya farasi karibu na eneo ambalo mbio za London marathon zitamalizikia Jumapili Aprili 21.
Askari wa ulinzi wa Marekani wakilinda doria katika kituo kikuu cha usarifi cha New York, Grand Central Terminal, mjini humo April 16, 2013.
Polisi wa Boston police wakilinda eneo la uwanja wa Copley mjini Boston.