Marekani yamuwekea vikwazo kiongozi wa kijeshi wa Sudan

  • VOA News

Kiongozi wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan

Marekani imemuwekea vikwazo kiongozi wa jeshi la Sudan, ikitaja kuhusika kwake katika uhalifu wa kivita katika mzozo ambao umelitumbukiza taifa hilo lenye utajiri wa mafuta katika hali mbaya tangu mwaka jana, kusababisha njaa, kuua maelfu ya watu na kuwakosesha makazi mamilioni ya wengine.

Marekani imemchukulia vikwazo hivyo kiongozi huyo wa kijeshi wiki moja baada ya kumchukulia vikwazo mpinzani wake kwa vitendo ilivyovielezea kuwa mauaji ya kimbari.

Vikwazo vya Alhamisi dhidi ya Abdel Fattah Al-Burhan na kampuni inayoizuia silaha Sudan yenye makao yake Hong Kong, vinawazuia kuingia Marekani au kutumia njia za usafiri za Marekani na vinawazuia kupata mali zozote nchini Marekani.

Vikwazo hivyo vinasababisha pande zote mbili kukabiliwa na changamoto za kiuchumi katika mzozo ambao wizara ya mambo ya nje ya Marekani iliuelezea kama mzozo mbaya wa kibinadamu duniani, lakini athari zake hazitakuwa kubwa kutokana na uhusiano mbaya wa kidiplomasia na taifa hilo kubwa barani Afrika.