Marekani yamtambua mpinzani Venezuela kama Rais Mteule

Serikali ya Marekani, Jumanne imemtambua mgombea wa upinzani wa Venezuela, Edmundo Gonzalez, kama rais mteule wa nchi hiyo ya Amerika Kusini, miezi kadhaa baada ya Rais Nicolas Maduro kutangaza ushindi wa uchaguzi wa Julai.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alimtambua Gonzalez katika ujumbe wa X ambapo pia alidai kuwa ni heshima wapiga kura wa Venezuela.

Utawala wa Rais wa Marekani, Joe Biden umesema Gonzalez alipata kura nyingi zaidi katika uchaguzi ulipingwa wa Julai 28 lakini umeshindwa kumtambua kama rais mteule.

Tume ya uchaguzi ya Venezuela, ambayo ina maafisa wengi wafuasi wa Maduro, ilimtangaza Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi saa chache baada ya upigaji kura kumalizika.

Tofauti na uchaguzi kadhaa uliopita wa marais, mamlaka za uchaguzi hazikutoa hesabu za kina za kura.