White House imesema pesa zinazosalia zitatumiwa kuwapa fidia waathirika wa ugaidi uliofanywa na Taliban.
Rais Joe Biden alisaini amri ya kiutendaji kutangaza dharura ya kitaifa, ili kukabiliana na kudorora kwa uchumi wa Afghanistan .
Hatua hiyo imejiri saa chache kabla ya wizara ya sheria ya Marekani kuwasilisha mpango huo kwa jaji wa serikali kuu kuhusu nini cha kufanya na fedha hizo zilizoshikiliwa, kufuatia wito wa dharura wa wabunge wa Marekani na Umoja wa mataifa kutaka fedha hizo zitumiwe kushughulikia mzozo mbaya wa kiuchumi ambao ulizidi kuwa mbaya tangu Taliban wachukuwe madaraka mwezi Agosti mwaka jana.
Maafisa wakuu wa utawala wa Biden wamesema watafanya kazi kuhakisha bilioni 3 na nusu ya pesa hizo zinazoshikiliwa na Marekani, zinawanufaisha wanainchi wa Afghanistan.