Tukio hilo limefanyika kwenye uwanjwa wa ndege wa kimataifa wa Abha nchini Saudi Arabia, akisema kwamba washirika wa kimataifa watawajibiisha waasi hao. Muungano wa vikosi unaoongozwa na Saudi Arabia na unaokabiliana na waasi hao tangu mwaka 2015, umesema kwamba watu 12 walijeruhiwa wakati wa tukio hilo, ingawa drone hiyo iilinaswa na vifaa vya angani.
Saa chache baadaye kundi hilo la waasi ambalo liliondoa serikali iliyokuwa ikitambuliwa kimataifa lilikiri kufanya shambulizi hilo. Sullivan alisema kwamba Saudi pamoja na washirika wa kimataifa watawaajibisha, kupitia taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani Alhamisi.
Aliongeza kusema kwamba kama Rais Joe Biden alivyomwambia mfalme Salman wa Saudi Arabia Jumatano, Marekani ipo tayari kulinda taifa hilo pamoja na watu wake dhidi ya mashambulizi.