Marekani yakamilisha sheria inayopiga marufuku magari ya umeme kutoka China na Russia

  • VOA News

Picha hii inaonyesha magari ya umeme yanayosubiri kupakiwa kwenye meli kwenye bandari ya Suzhou, katika mkoa wa mashariki nwa China wa Jiangsu, Septemba 11, 2023. Picha ya AFP

White House inasema imekamilisha kuweka sheria za kukabiliana na teknolojia ya magari kutoka China na Russia ambazo zitapiga marufuku magari yote yanayotumia umeme kutoka nchi hizo mbili kuingia kwenye soko la Marekani.

Katika waraka wa White House unaoelezea uamuzi huo, utawala wa Biden ulisema Jumanne kwamba ingawa magari ya umeme yanaleta faida, kuingia kwa maadui wa kigeni kama vile China na Russia kwenye soko lao la usambazaji kunaleta hatari kubwa “kuwaruhusu wadau hawa wabaya kufikisha mifumo hii ya umeme na data wanazokusanya.”

“Wizara ya biashara imetangaza sheria ya mwisho ambayo itapiga marufuku uuzaji na uagizaji wa programu na mifumo ya kielektroniki ya magari ya umeme, kutoka China na Russia, “waraka wa White House umesema.