Marekani yaituma tena manuari yake bahari ya Atlantic kuidhibiti Russia

Admirali John Richardson

Jeshi la Majini la Marekani Ijumaa limeimarisha uwepo rasmi wa manuari yake ya kivita, 2nd Fleet, ikiimarisha ulinzi upande wa Kaskazini mwa bahari ya Atlantic ambapo jeshi la Russia linafanya operesheni za kivita katika kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa Vita Baridi vya Dunia.

Mabadiliko hayo kwa sehemu kubwa ni ya kiutawala. Imemrudisha msimamizi mwenye cheo cha admiral atakaye husika kusimamia manuari za kivita zote za Marekani wakati zikiendelea kulinda eneo kati ya Pwani ya Mashariki ya Marekani na Bahari ya Barents, iliyoko nje ya pwani ya Norway na Russia.

Kurudishwa kwa manuari hiyo inaonyesha mabadiliko makubwa katika mkakati wa jeshi la Marekani. Jambo la msingi linalozingatiwa ni kuhama kutoka katika vita ya ugaidi, Mashariki ya Kati, na kuangalia ushindani unaozidi kupamba moto kati yake na Russia na China.

“Sisi hatutaki vita,” Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Majini Admirali John Richardson amesema akiwa katika manuari ya kivita USS George H. W. Bush inayobeba ndege za kivita huko Norfolk, Virginia.

Lakini njia ya kipekee kuepusha vita ni kadiri inavyo wezekana kuendeleza nguvu ya juu kabisa na hatari na zenye ubora katika jeshi la majini,” amesema mkuu huyo.

Richardson ameongeza kusema kwamba iwapo itahitajika, manuari ya 2nd Fleet “ itafanya operesheni ya mashambulizi muhimu kumtokomeza adui yoyote.”