Marekani yaitaka Iran itambue haina maslahi na hali ya Mashariki ya Kati

  • VOA News
Marekani imekuwa ikizitaka nchi kupitia ushirikiano wake wa kidiplomasia kuiambia Iran kwamba kuongezeka kwa mvutano Mashariki ya Kati sio maslahi yake, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller amesema Jumatatu.

Akizungumza katika mkutano wa kila siku, Miller amesema huu ni wakati muhimu kwa eneo hilo na kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, amekuwa katika mawasiliano ya kusaidia kutuliza mvutano huo, lakini pia amesema Washington inajiandaa kwa uwezekano wowote.

Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, aliuwawa katika mji mkuu wa Iran Tehran wiki iliyopita, shambulizi ambalo limeibua vitisho vya kulipiza kisasi kwa Israel na kuzua wasiwasi zaidi kwamba mzozo wa Gaza unageuka na kuwa vita vya Mashariki ya Kati.

Iran imeilaumu Israel na kusema itaiadhibu licha ya Israel kutosema kama imehusika na mauaji hayo.