Marekani yaisaidia Sudan Kusini kuendeleza sekta ya sheria

Watu wenye silaha wakitembea katika maeneo ya mpaka wa Sudan kaskazini na kusini .

imetangaza msaada wa dola milioni mbili ikiwa ni juhudi za kusaidia Fedha zilizotolewa zitatumika kuwapatia mafunzo majaji na watu wengine katika sekta ya sheria huko Sudan Kusini.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza msaada wa dola milioni mbili ikiwa ni juhudi za kusaidia kuwapatia mafunzo majaji na watu wengine katika sekta ya sheria huko Sudan Kusini.

Fedha hizo zitapelekwa kwenye taasisi ya kimataifa ya maendeleo ya sheria yenye makao yake Rome, taasisi ambayo imeanzishwa na mawakili ili kuhamasisha fani ya sheria katika mataifa yanayoendelea.

Wizara imesema mchango wake utasaidia katika kufungua shule ya sheria Sudan Kusini, kuwa na kituo cha msaada wa kisheria na kuwapatia mafunzo majaji na wahitimu wa karibuni wa fani ya sheria ambao wanapanga kufanya kazi kama wanasheria.

Katika kura ya maoni ya mwezi Januari, watu wa Sudan Kusini walipiga kura kwa idadi kubwa kutaka kujitenga na kaskzini ili kuunda taifa jipya ambalo litaitwa Sudan Kusini.