Marekani imezieleza Iran na Israel kwamba migogoro ya Mashariki ya Kati haipaswi kuongezeka, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amesema Jumanne, huku kukiwa na hofu kwamba Tehran na washirika wake wanajiandaa kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israeli.
Maafisa wamewasiliana mara kwa mara na washirika katika ukanda huo na makubaliano ya wazi yamefanyika kwamba hakuna anayepaswa kuzidisha hali hiyo, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani amesema.
“Tumekuwa tukishirikiana katika diplomasia ya juu na washirika, tukiwasilisha ujumbe huo moja kwa moja kwa Iran na Israeli,” Blinken amesema.
Marekani itaendelea kuilinda Israel dhidi ya mashambulizi, Blinken alisisitiza, lakini akabainisha kuwa kila upande katika eneo hilo anapaswa kuelewa hatari za kuongezeka mvutano na kuto tafakari adhari zake kwa kina.