Marekani yaidhinisha chanjo ya pili ya Covid 19

Kampuni ya madawa ya Moderna ikihifadhi utaratibu wa chanjo za COVID-19 katika kituo chao huko Hollywood, Florida, Aug. 13, 2020.

Jopo moja la Marekani limeidhinisha utumiaji wa dharura wa chanjo ya pili ya COVID-19 siku ya Alhamisi.

Kamati ya washauri huru na wataalam wa Idara ya Chakula na Madawa ya Marekani (FDA) ilipiga kura, baada ya majadiliano ya saa saba, kupendekeza utumiaji wa chanjo iliyotengenezwa na Mtengenezaji wa dawa wa Marekani Moderna, wiki moja baada ya wasimamizi wa serikali kuu kuidhinisha chanjo ya kwanza ya matumizi ya dharura .

Ushahidi ambao umesomwa kwa kina juu ya chanjo hii unazidi sana changamoto zozote ambazo tumeona, Dk Hayley Gans, Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Stanford, alisema Alhamisi.

Habari hizi zinakuja wakati Marekani imerekodi karibu vifo 310,000 kutokana na virusi hivyo, kulingana na Kituo cha taarifa za virusi vya corona kutoka Johns Hopkins.

Kuna zaidi ya visa milioni 1.6 vilivyothibitishwa vya COVID-19, nchini Marekani.

Idhini ya FDA ya matumizi ya dharura ya chanjo inaweza kupatikana mapema Ijumaa.